Kwa mujibu wa gazeti la Al Masr al Youm, al Taib aliyasema hayo hivi karibuni alipohutubu mahfali ya kuwatunuku shahada wanachuo waliofuzu katika chuo hicho na kuongeza kuwa: "Vatican inashirikiana na wanaopinga dini katika ulimwengu wa Magharibi kushambulia misingi ya ustaarabu wa Kiislamu".
Mwanazuoni huyo wa Al Azhar ametoa wito kwa Waislamu kutumia fikra, hekima na nidhamu katika hotuba za Kiislamu katika kueneza dini.
Dr. Ahmad Taib amesema. Al Azhar si taasisi ya Tabligh au kutangaza dini bali ni taasisi huru ya kutoa mafunzo na haipaswi kukubali kutumiwa kisiasa na serikali. 342880