Kwa mujibu wa mtandao wa Intaneti wa Al Furat, Afdhal as-Shami Naibu Mkurugenzi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS amesema kuhusu suala hilo kuwa: " Wakristo na Wasabii wengi nchini Iraq wanashiriki katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Abu Abdillah Hussein AS katika mji mtakatifu wa Karbala".
Ameongeza kuwa Wakristo wakiwa wamebeba bendera nyeusi wamejiunga na Waislamu katika maombolezo hayo.
Afdhal as-Shami amebainisha kuwa: "Mbali na Waislamu Mashia, Waislamu wa madhehebu ya Sunni pia wameshiriki katika maombolezo hayo pamoja na Wakristo na Wasabai".
Naibu Mkurugenzi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS amesema kuwa: "Kushiriki wafuasi wa dini na madhehebu mbalimbali katika maombolezo ya Aba Abdillahi Hussein AS ni jambo linalodhihirisha ujumbe wa kimsingi na wenye thamani kubwa wa harakati ya kupigania uhuru ya Imam Hussein AS, kiongozi wa mashahidi".
Wasabai ni kundi la Wairaqi ambao itikadi na mila zao zinafungamana na maji. Kundi hili ni kati ya wakaazi wa kwanza kabisa wa ardhi ambayo zama za kale ilijulikana kama Bain Nahrein (Mesopotamia). Wanaamini kuwa maji ndio chimbuko la kuwepo na mwanzo wa maisha. Leo aghalabu Wasabai wanaishi kusini mwa Iraq karibu na mito mikubwa ya Iraq. 342955