IQNA

Ayatullah Subhani:

Nyota ya Wazayuni imo katika hali ya kuzama

9:44 - January 05, 2009
Habari ID: 1727648
Mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ja’far Subhani ametoa taarifa akilaani jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na akasema, nyota ya Wazayuni imo katika hali ya kuzama.
Taarifa hiyo imesema kuwa mwaka 2009 umeanza sambamba na umwagaji damu wa Wazayuni katika Ukanda wa Gaza huku mauaji ya kizazi, ukatili dhidi ya wanawake na watoto na vitendo vya jeshi la utawala ghasibu vya kuharibu miundo mbinu na taasisi muhimu za wananchi wa Gaza vikiendelea na nchi za Kiarabu na Kiislamu zikishuhudia tu kwa macho jinai hizo.
Ayatullah Subhani amesema: Ushahidi unaonyesha kuwa kuna aina fulani ya mapatano kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi jirani ambazo zimeuruhusu utawala huo ghasibu kutekeleza mauaji dhidi ya taifa madhlumu la Palestina huko Gaza na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo kuwaokoa wakazi wanaozingirwa wa Gaza kutoka kwenye baa la njaa na ukosefu wa madawa.
Taarifa hiyo imesema kuwa, jinai hizo zilizoanza mwishoni mwa mwaka 2008 zimekariri mauaji ya umati ya Waislamu wa Kipalestina huko Dir Yassin hapo mwaka 1948 ambapo Wazayuni waliwaua kinyama wanawake na watoto wadogo 900 na kukanyaga kanyaga miili yao kwa vifaru. Imesema, inasikitisha kwamba jinai hiyo imesahaulika kadiri muda unavyopita. Ayatullah Subhani amesema kuwa, hakuna dini yoyote ya mbinguni au mfumo wa kibinadamu unaoruhusu mashambulizi kama hayo yasiyokuwa na mpaka.
Taarifa ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu imesisitiza kuwa, japo utawala ghasibu wa Israel umelewa madaraka na kiu ya kuua watu, lakini unapaswa kuelewa kwamba, nyota yake imo katika hali ya kuzama.
Ayatullah Subhani amesema kuwa, ni wadhifa wa Kiislamu na kimaadili wa nchi zote za Kiislamu na wafuasi wa dini za mbinguni kukabiliana na jinai hizo na kulisaidia taifa lililokandamizwa la Palestina. Vilevile ni wajibu wa Umoja wa Mataifa, jumuiya za kutetea haki za binadamu na taasisi nyinginezo zinazoshughulikia masuala ya kibinadamu kutumia uwezo wao kuzima moto huo na kutibu majeraha ya maelfu ya Wapalestina.
Ayatullah Ja’far Subhani amesema kuwa moyo wa kupenda mwanadamu unawawajibisha Wakristo kote duniani ambao wanajitambulisha kuwa wafuasi wa Issa Masiya kugawana furaha zao na wananchi wanaodhulumiwa wa Gaza na kuchukua hatua za kimatendo za kuwatete badala ya kufurahia. Aidha wanapaswa kudhihirisha wazi nembo ya upendo ya dini ya Issa Masih (as).
811253
captcha