Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yatajumuisha barua, simulizi fupi, na mashairi.
Washiriki katika maonyesho hayo wanaombwa kutuma maandishi yao katika faili lililoandikwa kwa mfumo wa Word kupitia barua pepe au email ifuatayo: diareranj@gmail.com
Siku ya mwisho ya kutuma maandishi ni tarehe 11 February 2009. Washindi watapata zawadi za kuvutia.
Maonyesho haya yanakusudia kuonyesha ufungamano na watoto wa Ukanda wa Gaza ambao wanakabiliwa na mateso na ukatili wa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.
Itakumbukwa kuwa mamia ya watoto wameuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa katika hujuma inayoendelea ya Wazayuni huko katika Ukanda wa Gaza. 344420