Maandamano hayo yalihudhuriwa na zaidi wanachuo 500 wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Jamiatul Moustafa (saw) ambalo walijumuika mbele ya ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Qum kusini mwa Tehran.
Katika mahojiano na IQNA, Iman Adili Katibu wa Harakati ya Wanafikra Dhidi ya Uzayuni katika chuo hicho amesema, wanachama wa jumuiya hiyo wameitisha maandamano kulalamikia kimya cha mashirika ya kimataifa mbele ya jinai za Wazayuni huko Gaza.
Maandamano hayo yamejumuisha wanachuo kutoka nchi 100 ambao wamezitaka serikali na umma mzima wa Kiislamu kuungana katika kuwasaidia wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Sheikh Mirzai ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Jamiatul Moustafa (saw) amesema kuwa watu wa Gaza kwa mara nyingine watatoa kipigo kwa utawala wa Kizayuni. Katika maandamano hayo mwakilishi wa kila nchi alitoa taarifa kuhusu harakati zinazofanyika katika nchi yake kuwasaidia Wapalestina huko Gaza. 344511