IQNA

Mnara wa Kituo cha Kiislamu wazinduliwa Solothurn, Uswisi

10:11 - January 11, 2009
Habari ID: 1729094
Mnara wa kituo cha Kiislamu cha mji wa Solothurn Kaskazini Magharibi mwa Uswisi umezinduliwa Jumamosi katika hafla iliyohudhuriwa na mubalighina na maimamu wa misikiti nchini humo.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Arab Online, ujenzi wa mnara wa msikiti huo mweupe wenye hati za dhahabu ulianza miaka minne iliyopita. Waislamu waliowachache nchini Uswisi walipoanza ujenzi wa mnara huo walikabiliwa na upinzani na malalamiko makali ya vyama vya kisiasa vyenye misimamo mikali vya mrengo wa kulia.
Mnara huu umejengwa kwa misaada ya waumini na Jumuiya za Misaada ya Kiislamu za Uswisi. Kituo cha Solothurn kitakuwa kituo kikubwa zaidi cha Kiislamu nchini Uswisi ambacho kila siku huwa mwenyeji wa Waislamu wengi ambao hufika hapo kuswali.
Kwa mujibu wa Farhad Afshar wa Jumuiya ya Umma, ujenzi wa mnara huo unakusudia kuonyesha utajiri wa utamaduni wa Kiislamu.
Kitakapokamilika kituo cha Kiislamu cha Solothurn kitajumuisha ukumbi wa mkutano, hoteli, jumba la makumbusho, ofisi na msikiti.
Kuna karibu Waislamu laki nne Uswisi nchi ambayo ina idadia ya watu takriban milioni 7.4. Asilimia 43 ya Waislamu wa Uswisi wana asili ya Uturuki.
Dini ya Kiislamu inahesabiwa kuwa ya pili nchini humo baada ya Ukristo. Hivi sasa kuna misikiti miwili tu iliyo na minara nchini Uswisi huko Zurich na Geneva. 345827
captcha