IQNA

Awamu ya mwisho ya mashindano ya sira ya Mtume Saudi Arabia

13:42 - January 12, 2009
Habari ID: 1729662
Awamu ya mwisho ya mashindano ya wanafunzi ya kuhifadhi sira ya Mtume SAW imeanza katika shule za Saudi Arabia kwa hisani ya Wizara ya Elimu nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Ukadh la Saudia, awamu ya mwisho ya mashindano ya wanafunzi ya sira ya Mtume chini ya anuani ya “Amiri wa Naif” na kwa maudhui ya “Sira ya Mtume na Masomo ya Kiislamu” inafanyika kwa kuwajumuisha wanafuzni wa kike na kiume.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Mwamko wa Kiisalmu kitengo cha wanawake katika Wizara ya Elimu Saudia, Hasa al Waili amesema, lengo la kufanyika mashindano hayo ni kujaribu kutoa mafunzo kwa mabarobaro na kuwahimiza wahifadhi sunna ya Bwana Mtume na kuzitekeleza kivitendo katika maisha yao. Ameongeza kuwa malengo mengine ya mashindano hayo ni kuwahimiza wanafunzi kushikamana na mafunzo ya Kiislamu na kutumia wakati wao wa starehe kwa njia zinazofaa.
Matokeo ya mashidano hayo yatatangazwa tarehe 25 Muharram sawa na tarehe 22 Januari. 346205

captcha