IQNA

Mkutano wa kimataifa wa "Dini Baada ya Septemba 11"

14:50 - January 19, 2009
Habari ID: 1733069
Mkutano wa kimataifa wa Dini Mbalimbali Duniani Baada ya Septemba 11umeanza kazi zake katika mji wa New Delhi huko India.
Kiongozi wa Mabuddha Dalai Lama ambaye amehutubia katika ufunguzi wa mkutano huo ameashiria kushadidi hisia za uhasama na chuki dhidi ya Uislamu katika miaka ya hivi karibuni na akasisitiza kwamba taswira mbaya inayotangazwa katika vyombo vya habari kuhusu Uislamu si sahihi na kwamba Uislamu hauna uhusiano wowote na ugaidi.
Mkutano huo wa siku tatu unasimamiwa na Kituo cha Utafiti wa Sayansi ya Dini cha India, Jumuiya ya Kiislamu ya New Delhi na Kitivo cha Utafiti wa Masuala ya Kidini cha Chuo Kikuu cha McGill cha Canada.
Washiriki katika mkutano huo wanazungmzia uhusiano wa dini na mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali, vita na amani, elimu na teknojia, haki za binadamu, sana na maadili.
Suala jingine linalojadiliwa katika mkutano huo ni njia za kutatua migogoro ya kidini na mchango wa mazungumzo katika kutatua matatizo ya aina mbalimbali. 350452

captcha