IQNA

Nafasi muhimu ya maulamaa Waislamu barani Ulaya

11:38 - February 01, 2009
Habari ID: 1738443
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Uturuki amesema wasomi na wanafalsafa wa ulimwengu wa Kiislamu wamekuwa na mchango muhimu katika ustawi na maendeleo barani Ulaya.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kuwait, Muhammad Aidin ameyasema hayo alipohutubia wanahabari nje ya Bunge la Ulaya mjini Brussels Ubelgiji na kuongeza kuwa: “Wasomi na watafiti Waislamu katika zama za mwamko wa Ulaya (Renaissance) na marekebisho barani humo waliwasilisha kazi zenye thamani na kuandika vitabu vya kisayansi vilivyokuwa na mchango muhimu katika ustawi wa sayansi barani Ulaya”.
Muhammad Aidin ambaye anafunza falsafa na dini katika vyuo vikuu vya uturuki amesema kuwa, Uislamu unatoa himaya kwa fikra za kisayansi. Akiashiria mafanikio na ustawi wa ulimwengu wa Kiislamu katika karne za kati amesema kuwa hakuna mgongano wowote kati ya dini na elimu ya sayansi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Uturuki ambaye alipata cheti chake cha Udaktari wa filosofia katika Chuo Kikuu cha Edinburgh Uingereza, ameongeza kuwa: “Hatupaswi kuibebesha dini lawama za matatizo ya watu binafsi na kufeli kisiasa na katika masuala mengine”. 356371
captcha