Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu imesema kuwa, Barack Obama amemtumia barua Katibu Mkuu OIC Ekmeleddin Ihsanoglu akiahidi kufanya juhudi za kustawisha ushirikiano wa Marekani na jumuiya hiyo.
Rais Obama pia ameishukuru OIC kwa kumtumia ujumbe wa kumpongeza baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Marekani.
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu tarehe 21 Januari ilimtumia barua ya wazi Barack Obama ikimpongeza kwa kuapishwa kuwa Rais mpya wa Marekani na kueleza matumaini ya kuanza mazungumzo halisi kati ya nchi za Magharibi na ulimwengu wa Kiislamu.
Barua hiyo ilimtaka Obama kufanya jitihada za kuimarisha amani ya kweli kote duniani.
357961