IQNA

Spika wa Bunge la Iran aitaka Marekani kubadili mwenendo wake badala ya maneno

16:23 - February 16, 2009
Habari ID: 1744776
Spika wa Bunge la Iran ameitaka Marekani kubadili mwenendo na matendo yake kuhusu Iran badala ya kubadili maneno na lugha yake.
Dakta Ali Larijani ambaye alikuwa akihutubia waandishi wa habari wa kimataifa waliokuja nchini Iran kuakisi sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema matatizo ya Iran na Marekani si ya jazba na hisia ili yaweze kutatuliwa kwa maneno na hotuba za kuvutia bali yanahitaji mabadiliko ya kimatendo. Amesema nara za mabadiliko zilizotolewa na Rais Barack Obama wa Marekani pekee hazitoshi na kwamba badala ya kufanya mabadiliko katika maneno, Washington inapaswa kufanya mabadiliko halisi katika fikra na mwenendo wake.
Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa Marekani imefanya dhulma kubwa kwa taifa la Iran katika miongo kadhaa iliyopita na kwamba dhulma hizo zote zimesajiliwa katika historia. Aidha ameilaumu Marekani kwa matatizo makubwa iliyosababisha katika eneo la Mashariki ya Kati hususan huko Afghanista, Palestina, Lebanon na Iraq na akaikosoa nchi hiyo kwa kutekelza siasa za kindumakuwili katika masuala ya ugaidi, demokrasia na kadhia ya nishati ya nyuklia. Ameitaka Marekani kucheza mchezo wa sataranji na Iran badala ya kukunja ngumi na kupanda ulingo wa ndodi. 364154
captcha