IQNA

Wakfu chanzo cha kudumu mwanadamu

9:43 - February 26, 2009
Habari ID: 1748754
Mkurugenzi wa Idara ya Wakfu na Masuala ya Kheri katika wilaya ya Khomein, amesema kuwa kwa kuzingatia maneno ya maimamu watoharifu (as) kuhusiana na wakfu, suna hiyo humpelekea mwanadamu kuishi na kudumu milele.
Hujjatul Islam wal Muslimeen Sayyid Ali Imami amesema, wakfu ni suna nzuri ambayo inamuwezesha mwanadamu kutoa huduma nzuri kwa Waislamu wenzake. Amesema, licha ya kulinda mali zinazotolewa kwa ajili ya wakfu na kutekeleza nia ya wanaotoa wakfu hizo, lengo hasa la wakfu ni kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za kiutamaduni, kidini, kiafya, kitiba na kiustawi na kuandaa maonyesho ya vitabu vya kidini na hasa Qur'ani Tukufu misikitini. Amesema, malengo mengine ya wakfu ni kusaidia kufanyika vikao vya kidini, Qur'ani, kuwasaida wanafunzi wasio na uwezo, kutoa ardhi za wakfu kwa malengo ya elimu, kukarabatiwa maeneo ya kidini na kusimamia mabafu ya umma. 369422
captcha