Kwa mijibu wa kamati inayosimamia swala ya Ijumaa, ibada hiyo itaanza saa tano kwa kusomwa aya kadhaa za Qur'ani Tukufu, ambazo zitasomwa na Yusuf Afrosh, katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran. Baada ya hapo, Ali Asghar Yazdani, Naibu Waziri wa Elimu na Malezi wa Iran atazungumza mbele ya hadhara ya waumini kwa mnasaba wa kuwadia siku ya Masuala ya Malezi na Malezi ya Kiislamu nchini. Kisha Hussein Anwari, Msimamizi wa Kamati ya Misaada ya Imam Khomeini (MA) atapewa fursa ya kuzungumza, ikiwa ni katika kuwadia mwaka wa 30 wa kuasisiwa kamati hiyo muhimu.
Murtadha Tamaddun, Gavana wa Mkoa wa Tehran pia atazungumza katika ibada hiyo muhimu ambayo hufanyika kila siku ya Ijumaa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran. Kisha Adhana itaadhiniwa na Yusuf Afrosh na baadaye swala ya Ijumaa kuendeshwa na Ayatullah Hashimi Rafsanjani. 369429