IQNA

Kikao cha kuunga mkono taifa la Palestina chafanyika mjini Tehran

15:01 - March 05, 2009
Habari ID: 1752035
Kikao cha nne cha kimataifa cha 'Palestina Dhihirisho la Mapambano, Gaza, Mhanga wa Jinai' kilianza jana Jumatano mjini Tehran, ambapo wasomi, wanafikra, wanaharakati wa haki za binadamu na wataalamu mbalimbali wa masuala ya Palestina wanashiriki.
Miongoni mwa shakhsia muhimu wa ulimwengu wa Kiislamu ambao wamehutubia kikao hicho ni pamoja na Ayatullahil Udhma Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambaye dama amekuwa katika mstari wa mbele wa kutetea haki za taifa madhlumu la Palestina na Dakta Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu au Bunge la Iran. Maspika na Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizo za Kiislamu pia wanashiriki katika kikao hicho cha siku tatu.
Viongozi wa makundi mbalimbali ya mapambano ya Palestina pia wanashiriki katika kikao hicho.372516
captcha