IQNA

Rais Ahmadinejad asema:

Waislamu wanawajibika kufanya juhudi za kutekeleza malengo yao ya umoja

10:51 - March 19, 2009
Habari ID: 1757586
Moja ya misingi muhimu kwa ajili ya kufikia umoja na mashikamano baina ya Waislamu ni Waislamu kote duniani kutekeleza majukumu yao na kupiga hatua madhubuti zaidi za kufikia malengo yao.
Hayo yamesemwa na Rais Mahmuod Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkutano wa wanazuoni wa Kiislamu mkoani Kurdistan, kaskazini magharibi mwa Iran na akasisitiza kuwa Waislamu wana wajibu wa kufuatilia masuala yote ulimwenguni na mtu ambaye hafanyi jitihada za kuhakikisha malengo ya Mitume wa Mwenyezi Mungu yanafikiwa si Muislamu.
Amesema kuwa saada na ufanisi wa mwanadamu umo katika kumwabudu Mungu Mmoja, uadilifu na kufuata mafunzo ya Mitume.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaja kufikiwa kwa thamani na malengo ya Uislamu kuwa ni lengo la pamoja la Waislamu wote na akaongeza kuwa, hii leo Waislamu wanakabiliwa na hujuma kali mno za madui wa dini hiyo na iwapo wataghafilika kidogo ardhi zao zote zitakaliwa kwa mabavu.
Rais Ahmadinejad amesema kuwa utawala ghasibu wa Israel ndiyo hatari kubwa zaidi dhidi ya Uislamu na Waislamu na akasisitiza kuwa iwapo utawala huo utapewa fursa hautabakisha athari yoyote ya Kiislamu. 379534

captcha