Ameitaka serikali na bunge kujiepusha na masuala yanayozusha utata ili kufikia lengo hilo. Hayo yamesemwa na Ayatullah Hashimi Rafsanjani, mkuu wa baraza lililotajwa mbele ya umati mkubwa wa waumini waliofika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran kwa lengo la kutekeleza swala ya Ijumaa.
Mwanzoni mwa hotuba yake, Ayatullah Rafsanjani kama kawaida amewanasihi waumini kuzingatia takwa na uchaji-Mungu pamoja na umoja miongoni mwao. Ameashiria umuhimu wa misikiti katika muundo wa utawala wa Kiislamu na kusema kuwa athari za jambo hilo zimekuwa zikionekana wazi katika jamii.
Sheikh Rafsanjani amesema, neno "masjid" msikiti linatokana na kusujudu kwenye ardhi na kwamba misikiti ilikuwepo hata kabla ya kudhihiri Uislamu na kutolea mfano Msikiti wa al-Aqsa kuhusiana na jambo hilo. Amesema, misikiti ni msingi muhimu katika dini zote za mbinguni. Kwa msingi huo amesema kuwa misikiti haihusiana na zama wala kaumu moja tu bali inahusiana na zama na jamii zote zikiwemo za mwanadamu na majini.
Ayatullah Rafsanjani amesema jambo muhimu linalopasa kuzingatiwa kuhusiana na misikiti ni ikhlasi, ucha-Mungu, malezi na kuboreshwa kwa hali ya umma wa Kiislamu. Amesema misikiti haipasi kutumiwa kwa malengo ya kimaada na maslahi ya watu binafsi na kwamba kuchafuliwa kwa ibada ya Mwenyeiz Mungu na masuala kama hayo ni aina moja ya shirki.
Ayatullah Rafsanjani pia ametoa mkono wa pole kwa mnasaba wa kuaga dunia hivi karibuni, Bi Khadija, mke wa Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameashiria pia uchaguzi mkuu ujao wa rais nchini na kusema kuwa kwa mujibu wa sisitizo la Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi wa utawala wa Kiislamu wa Iran, wasimamizi na waandaaji wa uchaguzi huo wanapasa kupanga mikakati kabambe ya kuwavutia watu wengi kushiriki katika uchaguzi huo kwa sababu kura na maoni yao kuhusiana na viongozi wanaotaka kuwachagua ni suala muhimu katika kudumisha mfumo wa Kiislamu wa Iran.
Kuhusiana na ujumbe wa hivi karibuni wa Obama kwa serikali na taifa la Iran kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Kiiran, Ayatullah Rafsanjani amesema kuwa taifa la Iran halina tatizo lolote na taifa la Marekani bali na serikali ya nchi hiyo. Amesisitiza kwamba kama itabadili siasa zake za kiuadui dhidi ya Iran basi wananchi wa Iran pia watabadilisha siasa zao kuhusianana serikali hiyo. 380578