Amesema kuwa hatua za kinyama zinazofanywa na madola hayo haziwezi kuhuisha mzoga wa ubeberu duniani kwa sababu msingi wake umesimama juu ya siasa za chuki, tamaa na kiburi. Amesisitiza kwamba bila shaka ubeberu utatokomea tu ulimwenguni.
Rais Ahmadinejad amesisitiza kwamba leo hii jamii ya mwanadamu ina matumaini ya kujenga mustakbali mzuri lakini wale wanaofuatilia siasa za kudhulumu, uchokozi na kutoa mashinikizo makubwa dhidi ya mataifa mengine wamekuwa wakikata tamaa kila uchao.
Ahmadinejad ameashiria matamshi ya Rais Hugo Chaves wa Venezuela katika ufunguzi wa benki hiyo ya pamoja na kusema kuwa, hata kama kidhahiri sherehe hizo zimefanyika kwa ajili ya kufungua benki tu, lakini kwa hakika ni mwanzo wa ushirikiano mkubwa wa baadaye na ishara ya wazi ya azma thabiti ya pande mbili hizo kwa ajili ya kujenga dunia mpya.
Rais Mahmoudnejad amesema mwishoni kwamba hiyo ni alama ya matumaini na harakati kuelekea kwenye ushindi unaofuatiliwa kwa azma kubwa na mataifa mawili haya. 382288