Maelfu ya waandamanaji katika mji wa Istanbul walianza maandamano hayo siku ya Jumamosi liyopita wakibeba mabango yanayoitaka Marekani kuondoa majeshi yake huko Iraq na Afghanistan.
Waandamanaji hao pia walibeba mabango yanayopinga Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO na operesheni zake za kijeshi nchini Afghanistan. Vilevile walichoma moto bendera za Marekani na jumuiya ya NATO.
Maandamano kama hayo ya kupinga safari ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Uturuki yanafanyika pia katika miji mingine ya nchi hiyo.
Uturuki ndio nchi pekee ya Waislamu mwanachama wa jumuiya ya NATO na nchi ya pili yenye udadi kubwa ya jeshi katika jumuiya hiyo baada ya Marekani.
Rais Barack Obama wa Marekani aliwasili nchini Uturuki jana. 383149