IQNA

Kuanzishwa safari za ndege kuelekea mji wa Najaf

11:26 - April 22, 2009
Habari ID: 1768304
Gavana wa mkoa wa Ardebil amesema kuwa viongozi wa mkoa huo wanafanya juhudi za kuanzisha safari za ndege katoka mji wa Ardebil kuelekea mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq.
Hayo yamesemwa na Gavana Mansur Haqiqatpur ambaye ameongeza kuwa uchunguzi wa suala hilo umefanyika kufuatia udharura wa kuanzishwa safari mpya za ndege katika uwanja wa ndege wa Ardebil.
Gavana huyo ametangaza mipango ya kuanzisha safari hizo za ndege katika mazungumzo yake na Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Ndege la Mahan la nchini Iran. Gavana huyo amesema kuwa safari nyingine zitakazoanzishwa kutika uwanaj huo wa ndege ni zile zitakazoelekea katika miji ya Dubai na Kish. 392275
captcha