Sheikh Abdul Shakir Nurmatov anatazamiwa kuendelea na shughuli zake za kielimu na utafiti katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Jamhuri ya Kyrgyzstan sambamba na kuwa Imamu wa msikiti wa wilaya ya 12 ya mji wa Bishkek. Aidha atashughulikia masuala ya kila siku ya Waislamu ya kidini na kisheria.
Sheikh Nurmatov amekubali kuwa Imamu wa msikiti huo kufuatia ombi la mfadhili aliyesimamia ujenzi wake.
Kyrgyzstan ni nchi ya Kiislamu iliyo Asia ya Kati na haina njia ya kuingia baharani. Inapakana na Kazakhstan upande wa kaskazini, Uzbekistan upande wa magharibi, Tajikistan upande wa kusini magharibi na China upande wa mashariki.
Nchi hiyo ilijitangazia uhuru kutoka Shirikisho la Sovieti Agosti 31, 1991.
Zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu. Ingawa Kyrgyzstan haifuati sheria za Kiislamu lakini, Uislamu una nafasi muhimu katika siasa za nchi hiyo.
393373