IQNA

Allah Fadhlullah

Kulaani jinai za magaidi peke yake hakutoshi

10:34 - April 27, 2009
Habari ID: 1770389
Mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu nchini Lebanon Allamah Muhamamd Hussein Fadhlullah ametoa taarifa akisema kuwa haitoshi kulaani jinai zinazofanywa na magaidi na amesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua za kimatendo dhidi ya magaidi hao.
Ayatullah Fadhlullah amesema kuwa kulaani jinai za kigaidi kama milipuko ya hivi karibuni nchini Iraq hakutoshi bali wanazuoni wa kidini na jamii ya Kiislamu inapaswa kuchukua hatua na kuzuia jinai hizo.
Taarifa hiyo imesema kuwa operesheni za kigaidi nchini Iraq zimesababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia yoyote na kwamba shambulizi la hivi majuzi dhidi ya eneo la Kadhimain huko Iraq limeua na kujeruhi watu mia mbili waliokuwa wamekwenda kuzuru haram za Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw).
Allamah Fadhlullah amesema kuwa vitendo kama hivyo vinafanywa na makundi ya Kiwahabi yenye misimamo ya kufurutu mipaka ambayo yanawakufurisha Waislamu wengine. Amewataka Waislamu wote kuchukua hatua za kudhibiti makundi hayo. 394559

captcha