Katika ufunguzi wa maonyesho hayo uliofanyika baada ya kumalizika kikao cha wazi cha Bunge, Spika wa Bunge Ali Larijani alielekea katika ukimbi wa Aftab na kuzindua maonyesho hayo kwa mnasaba wa kukaribia tarehe pili Mei ambayo ni kumbukumbu ya siku ambayo Ayatullah Murtadha Mutahhari aliuawa shahidi.
Maonyesho hayo pia yanajumuisha CD za hotuba za msomi huyo bingwa wa Iran.
Shahid Mutahhari aliuawa Shahidi Mei Mosi mwaka 1979 katika hujuma ya kigaidi. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Februari mwaka 1979, Shahid Mutahhari alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na anahesabiwa kuwa mmoja kati ya wanafikra bingwa wa Kiislamu katika zama hizi. 396221