IQNA

Uislamu, dini ya kwanza nchini Albania

9:38 - May 06, 2009
Habari ID: 1774514
Uislamu ndio dini yenye wafuasi wengi zaidi katika nchi ya Albania. Karibu asilimia 75 ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika eneo la Balkan barani Ulaya, kuna Waislamu milioni 2.2 kati ya idadi ya watu 3.1 nchini Albania.
Baadhi ya takwimu zinasema, asilimia 70 ni Waislamu huku baadhi zikionyesha ni asilimia 75.
Aidha uchunguzi unaonyesha kuwa asilimia 25 ya Waislamu wa Albani ni wafuasi wa madhebu ya Ahlul Bait. Aghlabu ya Waislamu nchini humo ni Masunni na wanaishi katika miji mikubwa. Baada ya Waislamu, wanafuatia wafuasi wa madhehebu ya Kikristo ya Orthodox na baada yao Wakatoliki ndio wanaofuata kwa wingi. Wakatoliki wanaishi kaskazini mwa Albania huku Waorthodox wakiishi maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.
Waislamu wa Albania hawaishi tu katika nchi hiyo bali wamesambaa katika nchi nyinginezo za eneo la Balkan hasa Macedonia, huku wengine wakiwa katika nchi mbalimbali za bara Ulaya.
Albania ni nchi iliyo kusini-mashariki mwa Ulaya na inapakana na Ugiriki upande wa kusini-mashariki, Montenegro upande wa kaskazini, Kosovo upande wa kaskazini-mashariki na Macedonia upande wa Mashariki. Katika upande wa magharibi ina pwani katika bahari ya Adriatic na bahari ya Ionian upande wa kusini-magharibi. 399804

captcha