Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, chama hicho cha Kiislamu katika taarifa kwa bunge ya nchi hiyo kimesema: "Katika zama hizi, utamaduni wa kigeni unaingia nchini na kusambazwa miongoni mwa vijana kupitia njia mbali mbali za vyombo vya habari chini ya kisingizio cha demokrasia na hivyo kueneza utamaduni wa Kimagharibi uliojaa ufisadi wa kimaadili unaokinzana na thamani , mila na desturi za kidini na kitaifa za Jamhuri ya Azerbaijan". Chama cha Kiislamu cha Jamhuri ya Azerbaijan kimesema njia pekee ya kukabuliana na hujuma ya utamaduni potofu wa Kimagharibi ni kufungamana na mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Jamhuri ya Azerbaijan ni nchi iliyo katika eneo la Caucasus la Eurasia. Nchi hiyo iko katika makutano ya Asia Magharibi na Ulaya Mashariki. Inapakana na Bahari ya Caspian upande wa Mashariki, Russia upande wa kaskazini, Georgia upande wa kaskazaini-magharibi, Armenia upande wa magharibi na Iran upande wa kusini. Nchi hiyo ilijiondoa kutoka Shirikiso la Sovieti na kujitangazia uhuru mwezi Oktoba mwaka 1991. Uamuzi huo uliidhinishwa katika kura ya maoni mwezi Desemba mwaka 1991 wakati Shirikiso la Sovieti liliposambaratika. Zaidi ya asilimia 96 ya wananchi wote wa Jamhuri ya Azerbaijan ni Waislamu. 406081