Kongamano la kitaifa la "Mwanamke, Mapinduzi ya Kiislamu, Ujenzi wa Ustaarabu Mpya wa Kiirani-Kiislamu' litafanyika mwezi Desemba katika Kituo cha Utafiti na Masomo ya Wanawake Chuo Kikuu cha Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo litajadili sura halisi ya mwanamke Muislamu mwanafikra katika uga wa ustawi wa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni nchini Iran.
Aidha makala zitakazowasilishwa zitahusu masuala kama vile: 'utambulisho wa mwanamke Muislamu wa Iran na nafasi yake katika ustaarabu wa Iran na Kiislamu', 'mitazamo ya Imam na Kiongozi Muadhamu kuhusu utambulisho mpya wa mwanamke Muislamu Muirani', 'nafasi ya mwanamke katika ustaarabu mpya wa Kiislamu-Kiirani' na vile vile 'nafasi ya mwanamke katika usimamizi na uendeshaji masuala ya utamaduni'. 408484