IQNA

Ufilipino yaruhusu vazi la hijabu mahospitalini

12:14 - July 05, 2009
Habari ID: 1798637
Kamisheni ya Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali ya Ufilipino imesema kuwa serikali ya nchi hiyo imepasisha ruhusa na uhuru wa kutumia vazi la hijabu kwa wanawake wa Kiislamu katika hospitali zote za nchi hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwqa kufuatia juhudi za Jumuiya ya Kiislamu ya Madaktari wa Ufilipini. Kwa mujibu wa uamuzi huo ambao umepasishwa na Kamisheni ya Maaskofu wa Ufilipino, wanawake wa Kiislamu wanaofanya kazi katika hospitali sasa wanawesza kuhudumu wakiwa na vazi la hijabu hata katika hospitali za Kikristo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya ya Dini za Ufilipino amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa watu wote wana haki ya kutende kazi na shughuli zao kwa mujibu wa itikadi na imani zao za kidini. 429655

captcha