Maelfu ya Waislamu walikutana jana nchini Ujerumani kumkumbuka na kumsomea dua Marwa al Sherbini, mwanamke Muislamu wa Kimisri aliyeuwa kwa kudungwa kisu na raia Mjerumani katika mahakama ya mji wa Dresden tarehe Mosi Julai mwaka huu.
Marwa alikwenda mahakamani kuwasilisha mashtaka dhidi ya jirani yake mbaguzi alipigwa kisu mara 18 na kuuawa shahidi mbele ya baraza la mahakama, mume na mwaname mwenye umri wa miaka 3.
Marwa al Sherbini ametambulia na Waislamu katika nchi nyingi za Kiislamu kuwa ni Shahidi wa Hijabu kutokana ma kuuawa kwa sababu ya vazi lake la hijabu ya Kiislamu.
Serikali ya Ujerumani inalaumiwa mno kwa kutoonyesha msimamo madhubuti wa kulaani mauaji hayo. 431951