Kwa mujibu wa IQNA, tamasha hiyo imefanyika mjini Jakarta na imejumuisha qiraa, hifdhi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu, semina na vikao kuhusu masuala ya uchumi na mfumo wa benki za Kiislamu, biashara ya bidhaa halali, nafasi ya zaka katika uchumi wa Kiislamu na lishe katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitume ujumbe katika tamasha hiyo uliyojumuisha hafidh na kari wa Qur'ani Tukufu na vile vile kundi la qasida. Aidha ujumbe wa Iran ulikuwa na maonyesho ya kaligrafia ya Qur'ani Tukufu, majarida na vile vile programu za kisasa za kompyuta za Kiislamu. 631050