Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Tanzania, mpango huo unafanyika kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali nchini humo.
Kwa mujibu wa mpango huo, mayatima wanaohitajia misaada katika jamii watapewa futari katika maeneo mbalimbali. Mbali na yatima futari pia inatolewa kwa familia masikini, misikiti na taasisi za Kiislamu nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ubalozi wa Imarati mjini Dar-es-Salaam kwa ushirikiano na Hilali Nyekundu ya Imarati pia unchini Tanzania pia utagawa tende miongoni mwa Waislamu wa Tanzania.
632275