IQNA

Kikao cha Mazungumzo Baina ya Tamaduni chafanyika nchini Denmark

16:33 - August 24, 2010
Habari ID: 1980502
Kikao cha Mazungumzo Kati ya Tamaduni na Nafasi Yake katika Kuimarisha Uhusiano Baina ya Wananchi kinafanyika leo katika mji mkuu wa Denmark Kopenhagen.
Kikao hicho kinafanyika chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Denmark kikihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu (ISESCO) Abdul Aziz Othman al Tuwaijri, wanafikra, wahadhiri wa vyuo vikuu, masomi wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu.
Katibu Mkuu wa ISESCO amehutubia kikao hicho akizungumzia nafasi ya mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali katika kuimarisha amani na utulivu kwenye jamii mbalimbali.
Jumatatu ya jana pia al Tuwaijri alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Lene Espersen ambapo pande hizo mbili zimejadili njia za kuimarisha ushirikiano kati ya ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi. 640269

captcha