Mtandao wa webhaber umeripoti kuwa Ed Husiç ambaye ni mwanachama wa chama cha Leba cha Australia na Muislamu mwenye asili ya Bosnia amefanikiwa kupata kura nyingi za kiti cha binge katika mji wa Sydney.
Hadi sasa hakuna Muislamu aliyewahi kuwa mbunge nchini Australia na ushindi wa Ed Husiç umeyafurahisha mno makundi ya Kiislamu nchini humo.
Waislamu wanaishi nchini Australia kwa zaidi ya miaka 200 na idadi yao inafikia watu milioni moja. Waislamu wengi wa Australia wanaishi katika miji ya Melborn na Sydney.
Idadi ya misikiti, nyumba za ibada na shule za Kiislamu barani Australia ni kati ya 300 hadi 350. 640603