Kwa mujibu wa gazeti la Zaman la Uturuki, idara ya mazingira ya Denmark imefanya utafiti kuhusu athari za sauti ya adhana inayotoka katika vipaza sauti vya misikiti na kubaini kuwa sauti ya adhana haina matatizo yoyote.
Baadhi ya makundi ya watu wenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Denmark yalikuwa yameiomba idara ya mazingira nchini humo kutoa sharti la kupigwa marufuku adhana kupitia vipaza sauti kabla ya ujenzi wa misikiti. Hata hivyo idara hiyo ya mazingira, baada ya kufanya utafiti, imesema adhana haina madhara ya kisauti katika mazingira.
Zaidi ya Waislamu laki tatu wanaishi katika maeneo mbalimbali ya Denmark. 641585