IQNA

Imarati kujenga misikiti katika nchi masikini za Kiislamu

14:23 - September 04, 2010
Habari ID: 1987024
Meya wa mji wa Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ametangaza mpango wa kujenga misikiti na vituo vya Kiislamu katika nchi masikini za Kiislamu duniani.
Kwa mujibu wa gazeti la Imarati la Al-Itihad, Meya wa Sharjah Mhandisi Sultan Abdullah Al Mualla akizungumza katika kikao cha Baraza la Mji amesema ujenzi wa misikiti hiyo ni katika fremu ya mpango maalumu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wa kutoa misaada. Amesema ujenzi huo utagharamiwa kwa misaada ya wananchi, wafanya kazi wa Baraza la Mji wa Sharjah na vile vile wakuu wa serikali.
Mhandisi al Mualla ameongeza kuwa kuna mpango pia wa kukarabati na kujenga upya misikiti katika nchi masikini za Kiislamu.
647086
captcha