IQNA

Fikra za Kiwahabi zimepata ushawishi katika Chuo Kikuu cha al Azhar

18:00 - September 06, 2010
Habari ID: 1989014
Mtafiti, mwandishi na mhadhiri wa teolojia na falsafa katika Chuo Kikuu cha al Azhar cha Misri Ahmad Abdul Rahim al Sayih amesema kuwa fikra za Kiwahabi zimepata ushawishi katika chuo hicho na miongoni mwa wahadhiri wake kwa miongo kadhaa sasa.
Ahmad Abdul Rahim al Sayih ambaye alikuwa akijibu swali kwamba ni kwa nini mazungumzo na mijada ya kidini imefifia katika Chuo Kikuu cha al Azhar, amesema kuwa hapana shaka kuwa tangu wahadhiri wa chuo hicho walipoanza kwenda kufunza katika vyuo vikuu vya Saudi Arabia, fikra zilizopitwa na wakati na zilizo mbali na mafundisho na thamani za Kiislamu za Kiwahabi zilianza kupenya na kuingia katika fikra zao.
Mhadhiri huyo wa al Azhar amesisitiza kuwa Uwahabi umeweza kuingia na kuwa na ushawishi katika chuo hicho kwa kutumia gharama kubwa ya fedha na sasa wafusi wa fikra za Kiwahabi ndani ya chuo cha al Azhar wanatoa fatuwa na hukumu za kuwakufurisha na kuwanasibisha na bidaa Waislamu wengine.
Ahmad Abdul Rahim al Sayih amesisitiza kuwa kuna udharura kwa Wizara ya Wakfu ya Misri na Chuo Kikuu cha al Azhar kurekebisha na kutazama upya malezi na mafunzo yanayotolewa kwa walinganiaji. Ameongeza kuwa mahatibu wa misikiti, maimamu wa swala za Ijumaa na jamaa wanapasa kutumia hotuba za kidini kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuwaelimisha wananchi misingi ya uhusiano uliopo kati ya dini na maisha, uzalishaji, maendeleo na ustawi. 649307

captcha