IQNA

Hati kamili ya 'Familia katika Uislamu' yachapishwa

15:37 - September 25, 2010
Habari ID: 2000950
Kamati ya Kimataifa ya Kiislamu ya Mwanamke na Mtoto imechapisha Kati Kamili ya Familia katika Uislamu kwa ushirikiano wa wanazuoni wa fiqhi wa ulimwengu wa Kiislamu na chini ya usimamizi wa taasisi ya kidini ya al Azhar.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Muhit, hati hiyo imechapishwa baada ya kuhakikisha kwamba inaoana kikamilifu na misingi ya mafundisho ya Kiislamu, Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw).
Hati hiyo inajumuisha haki za Kiislamu, kijamii na kibinadamu za watoto zilizochunguzwa na kuchambuliwa na wanafikra za Kiislamu na kueleza mjadala wa harakati za kijamii za watoto.
Kamati ya Kimataifa ya Kiislamu ya Mwanamke na Mtoto itatuma hati hiyo katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kwa ajili ya kupasishwa na kutambuliwa rasmi kuwa marejeo ya shughuli zinazohusiana na masuala ya watoto ndani na nje ya ulimwengu wa Kiislamu hususan katika duru za kimataifa. 661588


captcha