Kongamano hilo limejadili masuala kuhusu fikra za kidini, tamaduni na amani kwa mtazamo wa Kiislamu na juhudi za kuleta amani duniani. Aidha washiriki wamejadili masuala kama vile ugaidi, umasikini, ubaguzi wa rangi na ukosefu wa uadilifu.
Kwa mujibu wa IQNA, kongamano hilo limehudhuriwa na washiriki kutoka Venezuela, Marekani, Canada na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Washiriki kutoka Iran walikuwa ni pamoja na Saeed Ameli wa Chuo Kikuu cha Tehran na mbunge wa zamani Elham Aminzadeh.
684479