IQNA

Wanawake Waislamu wakabiliane na propaganda za adui

18:25 - November 01, 2010
Habari ID: 2023734
Kwa kutumia propaganda chafu dhidi ya wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu, maadui wanajaribu kuonyesha kuwa wametengwa kwa hivyo ni jukumu la wanawake Waislamu kukabiliana na habari hizo potofu.
Hayo ni kwa mujibu wa Leila Mazboodi mkuu wa kitengo cha Kifaransa katika televisheni la Al Manar ya Lebanon. Akizungumza na IQNA, Bi. Mazboodi amesema kutokana na sera potofu za nchi za Magharibi za kuuhujumu Uislamu, wanawake Waislamu sasa wanakumbwa na wimbi la hujuma za kiutamaduni na kipropaganda.
Mwanahabari huyo wa Lebanon amesema kuwa vyombo vya habari vya Kiislamu vina jukumu muhimu la kukabiliana na habari potofu za maadui. Bi. Mazboodi amewataka waandishi habari wa kike wa Kiislamu kuzingatia maadili ya Kiislamu katika mavazi yao na kuongeza kuwa hijabu ni ishara muhimu ya kuheshimu mafundisho ya Kiislamu.
Aidha ametoa wito wanawake Waislamu ambao ni waandishi habari kushiriki katika sekta mbalimbali za kijamii, kisiasa, kidini na kiutamaduni kwani maadui wanatumia mbinumbali kumdunisha mwanamke Muislamu. Amesema kuna umuhimu kwa wanawake Waislamu ambao ni waandishi habari kukutana mara kwa mara ili waweza kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kukabiliana na njama za maadui wa Uislamu.
Itakumbukwa kuwa Semina ya Kwanza ya Kimataifa ya Wanawake Waislamu Waandishi Habari ilifanyika Tehran Oktoba 30. Katika semina hiyo waandishi habari kadhaa wa Ulimwengu wa Kiislamu walitunukiwa nishani kutokana na juhudi zao za kikazi.
685623
captcha