Hayo yamesemwa na Ismail Sufer, mwandishi magazeti wa Afrika Kusini ambaye aliwakilisha nchi yake katika maonyesho ya kimataifa ya magazeti na mashirika ya habari yaliyofanyika hivi karibuni mjini Tehran. Suder amesema nchi za Magharibi zinachukulia kuenea Uislamu kuwa tishio kubwa kwa maslahi yao haramu ya kimaada na kuongeza kuwa mashambulio ya kijeshi ya nchi hizo dhidi ya Afghanistan na Iraq na kisha kueneza nchini humo ufuska na siasa zilizo dhidi ya mafundisho ya Kiislamu ni dalili tosha ya kuthibitisha madai hayo.
Suder ametoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la al-Qalam lililoanzishwa miaka mingi mjini Durban kwa ajili ya kupambana siasa za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Gazeti hilo la Kiingereza ambalo huchapishwa katika kopi 40,000 kila siku ni la Waislamu wa Afrika Kusini ambalo hutolewa bure kwa Waislamu. Gazeti hilo huakisi masuala na shughuli za kisiasa, kijamii na kiutamaduni kwa lengo la kuimarisha thamani na umoja wa Kiislamu nchini humo. 687507