Hayo ni kwa mujibu wa washiriki katika kongamano la ‘Nafasi ya Uislamu katika Dunia ya Leo’ lililofanyika Rabat Morocco kati ya 2-3 Novemba.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu nchini Morocco amesema kuwa ‘kubadilishana mawazo baina ya wataalamu ni njia bora zaidi ya kuanza mazungumzo baina ya tamaduni kwa lengo la kutafuta suluhisho kuhusu baadhi ya masuala ya kidini kwa kufuata muongozo wa kielimu unaoepusha uhasama na tafsiri potofu’.
Washiriki wa kongamano hilo wamejadili njia za maingiliano na kustahamiliana kama nukta muhimu za kuzingatiwa na Waislamu katika nchi za Magharibi ili waishi kwa amani na kupata ustawi.
Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu nchini Italia Yahya Pallavicini amesema chanzo cha mgogoro baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu ni ukosefu wa ufahamu kuhusu Uislamu. Amesema Waislamu barani Ulaya wana jukumu la kuwaelimisha watoto wao na kutangaza dini ya Kiislamu katika nchi za Magharibi.
689594