IQNA

Mashia wa Saudia wazuiwa kutoa mafunzo ya Hija

10:47 - November 09, 2010
Habari ID: 2028193
Waku wa utawala wa Saudi Arabia wamewazuia Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Khobar kutoa mafunzo ya ibada ya Hija kwa Mashia wa mji huo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wakuu wa Saudia kwa miezi kadhaa sasa wamewaweka Mashia nchini humo chini ya mashinikizo makali. Mbali na kuzuia kusimamishwa sala ya Ijumaa katika mji wenye Mashia wengi wa Khobar, wakuu wa Saudi Arabia wamezuia pia uandaliwaji wa mafunzo maalumu ya Hija kwa Mashia wa mji huo.
Aidha maafisa wa usalama katika mji wa Khobar wamewasaili watu ambao nyumba zao zilikuwa zikitumika kutoa darsa za Hija.
Ijumaa iliyopita, maafisa wa usalama waliizingira nyumba ya Allamah Sayyid Baqir al-Nasir khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Khobar na kumzuia kwenda kuongoza sala.
691389

captcha