IQNA

Mkutano wa Kimataifa wa Hija kufanyika kesho Makka

11:52 - November 09, 2010
Habari ID: 2028520
Mkutano wa Kimataifa wa kila mwaka wa Hija utafanyika kesho katika mji mtakatifu wa Makka ukihudhuriwa na maulamaa na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu.
Katibu wa mkutano huo Hisham bin Abdullah al Abbas amesema kuwa Mkutano wa Kimataifa wa Hija unasimamiwa na Wizara ya Hija ya Saudia na utahudhuriwa na Waziri wa Hija Fuad bin Abdul Salam al Farisi, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa nchi hiyo Abdul Aziz bin Abdullah Al Sheikh, maulamaa na wanafikra wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duaniani.
Ameongeza kuwa mkutano huo ambao maudhui yake kuu ni 'maarifa katika hija' unafanyika katika jitihada za kutoa huduma bora kwa mahujaji, kuwawezesha kutekeleza vyema ibada ya hija na kutatua matatizo yao. 691785


captcha