IQNA

OIC yalaani kuendelea ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni Quds Tukufu

14:16 - November 10, 2010
Habari ID: 2029514
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Ekmeleddin Ihsanoglu ametoa taarifa akilaani hatua ya utawala wa kizayuni wa Israel ya kuruhusu ujenzi wa vitongoji zaidi vya walowezi wa Kiyahudi katika mji wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Taarifa hiyo ya OIC imetolewa baada ya viongozi wa utawala ghasibu wa Israel kutoa kibali cha ujenzi wa zaidi ya nyumba elfu moja katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Quds Tukufu.
Katibu Mkuu wa OIC amesema katika taarifa hiyo kwamba hatua hiyo ya Israel imekanyaga haki za wananchi wa Palestina na kukiuka sheria za kimataifa na makubaliano ya Geneva.
Ihsanoglu ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel una lengo la kuharibu kikanilifu utambulisho wa Kiislamu wa Quds Tukufu na kuufanya wa Kiyahudi.
Amesema kuwa lengo jingine la Wazayuni ni kuwatenga Waislamu wa Quds na kuwapa Wayahudi wenye misimamo mikali fursa ya kufanya watakalo. Amesisitiza kuwa hatua hiyo inakiuka sheria za kimataifa na kukabiliana na jamii ya kimataifa.
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ameitaka jamii ya kimataifa na nchi kubwa za Mashariki ya Kati kukabiliana na utawala wa Kizayuni kwa kuuwekea mashinikizo zaidi. 692749

captcha