IQNA

Wilders kufikishwa tena mahakamani

15:04 - November 13, 2010
Habari ID: 2031057
Mbunge mwenye misimamo ya kibaguzi wa Uholanzi Geert Wilders ambaye ametoa tena matamshi ya kuuvunjia heshima Uislamu katika mahojiano yake na jarida la Kijerumani la Der Spiegel atafikishwa tena mahakamani miezi michache ijayo.
Kwa mijibu wa kituo cha habari ya Hurriyet, Mahakama ya Amsterdam nchini Uholanzi imetoa hukumu kuhusu ombi la kufutwa kazi jaji wa faili la Geert Wilders ambaye yeye mwenyewe anatuhumiwa kwa kuuhujumu na Uislamu na kuhamasisha vitendo vya kuivunjia heshima dini hiyo na imewateuwa majaji wengine watatu watakaoshughulikia faili hilo.
Msemaji wa mahakama ya Amsterdam amesema kuwa kesi ya kushughulikia faili la mbunge huyo mwenye fikra za kibaguzi itasikilizwa hivi karibuni.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa mbunge huyo wa Uholanzi mwenye fikra za kibaguzi ambaye ametengeneza filamu ya Fitna inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu angali anashambulia na kuvunjia heshima dini hiyo tukufu licha ya kwamba amefikishwa mahakama mara kadhaa kujibu mashtaka yanayomkabili. Wiki iliyopita mbunge huyo alifanya mahojiano na jarida la Spiegel la Ujerumani akiushambulia Uislamu. Wilders amesema kuwa siasa mpya za Kansela wa Ujerumani dhidi ya Uislamu zinaoana na mitazamo yake. 694356
captcha