Kongamano hilo ambalo lilianza tarehe 18 Novemba litakamilisha kazi zake kesho.
Mufti wa Misri Sheikh Ali Gumaa amesema katika ujumbe uliosomwa na Ibrahim Najm katika kongamano hilo kwamba dini ya Kiislamu ni dini inayokwenda na wakati, kukidhi mahitaji ya kila zama na kukabiliana na changamoto mbalimbali. Amesema Wamagharibi wengi wanaihusisha fatuwa na matamshi hasi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na kuongeza kuwa fatuwa ni moja ya nyenzo muhimu za kufahamu uhusiano kati ya Uislamu na dunia ya sasa, na katika miongozo yao ya kidini mamufti huwa hawatosheki na turathi za kifiqhi bali hutilia maanani pia hali halisi ya maisha ya sasa katika kutoa fatuwa na mamuzi ya kidini. 698723