Watu wenye misimamo mikali ya Kiwahabi tarehe 18 Novemba walimpiga na kumvunjia heshima Sheikh Hassan al Baqshi, mwanazuoni na mwanaharakati wa Kishia wa Saudi Arabia katika msikiti mtakatifu wa Makka na hatimaye akatiwa nguvuni na askari usalama wa nchi hiyo.
Watu walioshuhudia wamesema kuwa Mawahabi walitumia mabavu kumzuia Sheikh al Baqshi kukaribia Maqam Ibrahim (as) karibu na Nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba, suala mabalo lilizusha malumbano na hatimaye kupigwa na kuvunjiwa heshima mwanazuoni huyo ndani ya msikiti mtakatifu.
Sheikh al Baqshi ambaye ni amiri wa msafara wa hija wa Waislamu wa mashariki mwa Saudi Arabia aliachiwa huru jana baada ya kuingilia kati baadhi ya maulamaa wa Kiislamu. 699843