Kikao hicho ni katika mfululizo wa vikali vya kiutamaduni na Kiislamu vinavyofanywa na jumuiya hiyo.
Kituo cha habari cha Islamic-events kimeripoti kuwa kikao hicho kinafanyika kwa lengo la kubainisha haki za familia kwa mujibu wa aya za Qur'ani na vyanzo vingine vya Kiislamu. Kikao hicho kinahudhuriwa na Hassan Amduni, mhadhiri wa chuo kikuu na mtaalamu wa masuala ya familia. Ajenda kuu za kikao hicho ni mjadala kuhusu jinsi ya kuchagua mwenza (mke au mume) katika mtazamo wa maulamaa wa Kiislamu, kulea watoto wadogo na wajibu wa wazazi katika kadhia hiyo.
Vikao hivyo vya mafunzo hufanyika kila wiki vikiwashirikisha wasomi wa Kiislamu. 703596