IQNA

Kongamano la kimataifa la Sira ya Mtume laanza Misri

15:58 - December 05, 2010
Habari ID: 2042673
Kongamano la kimataifa la Sira ya Mtume Muhammad (saw) lilianza jana tarehe 4 Disemba katika mji mkuu wa Misri, Cairo.
Kongamano hilo la siku mbili linalosimamiwa na Kitengo cha Historia na Utamaduni wa Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Cairo linahudhuriwa na maulamaa, wahadhiri na wanafikra kutoka nchi za Misri, Sudan, Saudi Arabia, Kuwait, Malaysia, India na Marekani.
Mkuu wa Kitengo cha Historia cha Chuo Kikuu cha Cairo Muhammad Saleh Taufiq amesema kuwa kikao cha jana kilijadili sira ya Mtume (saw) katika mfumo wa dunia ya sasa na uchumi wa Kiislamu katika zama za Mtume na mifumo ya kiuchumi ya sasa. Kikao cha pili cha kongamano hilo kinachofanyika leo kinajadili sababu za kuvunjiwa heshima sira ya Mtume baada ya matukio ya Septemba 11. 706887

captcha