Vikao vya mafunzo vilivyopewa anwani ya 'Hali ya Sasa ya Palestina, Jibu la Kiutamaduni na Kisiasa la Matatizo" vimepangwa kufanyika tarehe 10 Disemba mwaka kesho mjini Paris, Ufaransa.
Vikao hivyo vitasimamiwa na Chuo cha Utafiti wa Masuala ya Kijamii cha Ufaransa (EHESS) kwa shabaha ya kuchunguza siasa za kiutamaduni za Palestina mkabala wa hujuma za kiutamaduni za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Vikao hivyo ambavyo vitaendelea kwa siku kumi vitahudhuriwa na wahadhiri na wasomi Waislamu na wasokuwa Waislamu wa Chuo cha Utafiti wa Masuala ya Kijamii cha Ufaransa (EHESS).
Makala zilizowasilishwa hadi sasa kwa ajili ya vikao hivyo zinahusu kumbukumbu ya mashahidi wa Sabra na Shatila, uchunguzi wa kihistoria na kiutamaduni wa utambulisho wa Palestina, turathi ya kiutamaduni ya Palestina na shughuli za kiutamaduni za waandishi habari wa Kipalestina kuhusu vita. 707404