IQNA

Wapalestina wanamiliki asilimia 12 tu ya ardhi ya Quds

20:54 - December 08, 2010
Habari ID: 2044826
Katika hali ya sasa Wapalestina wanamiliki asilimia 12 tu ya ardhi tukufu za Quds Mashariki na sehemu nyingine ya eneo hilo imeghusubiwa na Wazayuni.
Asilimia 38 imetumiwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi na asilimia nyingine 50 zinatayarishwa kwa ajili ya ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni.
Kituo cha habari cha Palestine Info kimeripoti kuwa katika mwongo uliopita Wazayuni walibomoa nyumba 995 za wananchi wa Palestina, na Wapalestina 5783 wakiwemo watoto 310 wamefanywa wakimbizi katika maeneo yanayokaliwa kwa amabavu. Takwimu hizo zimechapishwa katika kitabu kilichopewa jina la Baitul Muqaddas katika Makucha ya Wazayuni.
Sehemu moja ya kitabu hicho inasema: "Baada ya kukaliwa kwa mabavu eneo la Quds Tukufu katika kipindi cha baina ya 1967 na 1984 hakuna ruhusa yoyote iliyotolewa kwa Wapalestina kwa ajili ya ujenzi na tangu wakati huo vimetolewa vibali 33 tu vya ujenzi wa nyumba kwa Wapalestina. Takwimu hizo zinasema kuwa Wapalestina sasa wanamiliki asilimia 12 tu ya ardhi ya Quds Mashariki na zilizosalia zimeporwa na Wazayuni maghasibu.
Kitabu hicho pia kinatoa ripoti fupi kuhusu historia ya kuharibiwa nyumba na makazi ya Wapalestina na hatua zilizochukuliwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika uwanja huo. Kimesema kuwa tangu mwaka 2000 hadi sasa Wazayuni wameharibu yapata nyumba 1000 za wananchi wa Palesina katika mji mtakatifu wa Quds. 709285
captcha