IQNA

Masuni katika maombolezo ya Muharram nchini India

12:52 - December 09, 2010
Habari ID: 2045007
Waislamu wa madhehebu ya Suni nchini India katika jimbo la Uttar Pradesh wanafanya majlisi za kuomboleza kuuawa shahidi Imam Hussein AS na masahaba zake.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maombolezo hayo yanafanyika katika Shule ya Uthmaniya kaunzia Disemba 7 na yataendelea hadi siku ya Ashura, tarehe 10 Muharram.
Majlisi hizo zimeandaliwa na Jumuiya ya Uthmaniya katika eneo la Zangipur.
Sarafraz Ahmad aliyesoma katika Chuo Kikuu cha Baghdad anatoa mihadhara yenye anuani ya 'Tunayojifunza katika Maisha ya Mtume SAW".
Waislamu wa madhehebu ya suni nchini India hufunga saumu katika siku ya Ashura kama njia ya kufungamana na subira ya Imam Hussein AS na familia za mashahidi wa Karbala.
708630
captcha